Hakika sifa zote ni za Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi
Ndugu zangu katika imani kabla ya kuwapa hukmu ya siku kama hii ya Valentine hatuna budi kujua ya kua sisi wa Islamu tuna mambo yetu na siku kuu zetu kulingana na mfumo wetu wa ki islamu, nawao makafiri wana mambo yao na siku kuu zao kulingana na mfumo wao wakikafiri, nimakosa makubwa sisi waislamu kuingia au kushiriki katika mifumo yao ambao inaenda kinyume na itikadi yetu ya kiislamu ndipo makureshi walipokuja kwa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). kumuomba ashiriki katika mfumo wao wa kiibada Allahu Subhaana-hu Wa Ta'ala aliteremsha jawabu kutoka mbinguni moja kwa moja kuja kwa bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). awajibu na awaambie لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ Yakua nyinyi muna mfumo wenu na mimi nina mfumo wangu. Ikiwa mfumo wenu una waruhusu kufanya hivyo basi mimi wangu hauniruhusu kufanya hivyo kwa hivyo ndugu zangu waislamu nilazima tukae tukijua na kuelewa yakua maadamu twai-shi na makafiri hawatoridhika kuishi na wao tukiwa tumeshikilia mfumo wetu wa kiislamu mpaka watajaribu kutughuri sisi kuutupa mfumo wetu wasawa na kufuata mfumo wao muovu kama vile anavyo tuelezea Allahu Subhaana-hu Wa Ta'ala akisema kwenye qurani tukufu
وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ
Kwamba hawatoridhika mayahudi na manaswara mpaka tuwe ni wenye kufuata mfumo wao, ndipo bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). akatutaha-dharisha na kuwaiga wao au kujifananisha nawao ili tusiwe kama wao tukatupa uislamu wetu. Akasema Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam).
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهماأن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
ليس منا من تشبه بغيرنا لاتشبهوا باليهود ولا بالنصارى }الترمذي{
Imepokewa na Abdillah ibn Omar (RadhiaAllahu Anhu)kwamba bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). amesema si miongoni mwetu sisi ambae ana jifananisha na wasio kua waislamu musijifa-nanishe na mayahudi wala manaswara. (tirmidhi)
Kwa hivyo katazo hili limekuja moja kwa moja kwa waislamu hatuna budi kukatazika na katazo hili la Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). isije ika-tufikia sisi adhabu kali itokao kwa Allahu Subhaanahu Wa Ta'alae kwa sababu ya kukhalifu amri ya bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). kama anavyosema Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala kwenye qurani tukufu
فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“wajitahadhari wale wanao enda kunyume na amri ya bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). isije wafikia wao balaa kubwa kutoka kwa Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala au adhabu iliyo kali”. Kwa hivyo haina haja sisi kujiingiza katika sikukuu zao kama hizi za laana zenye kuchangia maasi na munkarati tofauti kama unywaji wa tembo na uzinifu bali tutosheke na siku kuu zetu alizokuja nazo Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). Kuhusu siku kuu zetu twaelezewa kwenye hadithi kama hii
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كان لأهل المدينة في الجاهلية يومان في كل سنة يلعبون فيهما فلما قدم النبي صلى الله عليه وسلم المدينة قال: كان لكم يومان تلعبون فيهما وقد أبد لكم الله بهماخيرا منهما يوم الفطر ويوم الأضحى
Imepokelewa na Anas bin Malik (RadhiaAllahu Anhu) akisema kulikua kwa watu wa madina katika zama za ujahili sikumbili kila mwaka wakicheza ndani yake na kusherehekea. Alipofika Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). mji wa madina aliwaambia watu wa mji wa madina ya kua mulikua na siku mbili mukicheza ndani yake naku-sherehekea na Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala amewabadilishia siku mbili hizo kwa siku mbili bora za Idi nazo ni siku kuu ya Idul’fitri na siku kuu ya Idul’adh’ha Kwa hivyo ndugu muislamu kwa hadithi hii twapata kuona yakua Uislamu pia una siku kuu zake ambazo zimewekewa waislamu waweze kusherehekea na kufura-hia zinapofika siku kuu kama hizo. Kwa hivyo haifai kwetu sisi kujiingiza kwenye siku kuu zao kama hizi ambazo zinaenda kinyume na mfumo wetu wa kiislamu. Kwa sababu lau sisi waislamu tutaziangalia siku kuu zao kama hizi kwa mtizamo wa kisawa sawa tutaona yakua ni siku kuu zenye kuleta uharibifu mku-bwa kwenye mujtamaa wetu wa kislamu. Si chrismas si valentine si pasaka day au happy new year hizi zote ni siku kuu ambazo zinaenda kinyume na Uislamu na kukhalifu muongozo sahihi wa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). tuchukue mfano mdogo wa siku kuu kama hii ya valentine twaona yakua ni siku kuu ambao ina shajiisha uzinifu na kuupa nguvu kwa kila njia nakuweza kuhimiza kila mtu awe na wake. Siku kama hi asipite patupu. Yani maana yake mvulana awe na girlfriend na msichana vile vile awe na boyfriend ili wapate kufanya mapenzi yao ya kiholela holela wakiita siku kama hii ya kua ni siku ya wapendanao ili watimize haja zao za kimapenzi. Natija inao patikana siku kama hii ni kuleta uharibifu kwenye umma na magonjwa mabaya ya nao tokea-na na vitendo vibaya vya uzinifu na ndipo Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). akasema
kwenye kauli yake
ماظهرت الفا حشة في قوم حتى يعلنوا بها إلاابتلوا بها با لطوا عين والأوجاع لم تكن في أسلافهم الذين مضوا من قبل
Yakua “Hapa tadhihiri uovu kwenye watu mpaka wakawa wanautangaza isipokua mwenyezi mungu atawapatia mtihani wa ugonjwa wataun yani kwa lugha nyengine leprosy na njaa kali ambao mambo hayo haya kua kwenye umma ulio tangulia”. Na hii ndivyo twaona magonjwa mabaya yalivyo enea kwenye ulimwengu kama huu ambao umma uliyo pita hawa kupata magonjwa kama haya ya leo.
Ndugu muislamu sidhani kwamba kuna mtu asiejua kisa cha valentine ama sababu kubwa makafiri kuweza kusherehekea siku kama hii ambao inakuja kila mwaka tarehi 14 February.
Kwa ufupi katika karne ya tano kanisa la catholic church lilitaka kubadilisha mila au desturi ya kiromani ambao kuanzia karne ya nne, wa kiristo wote walikua wa kiifuata mila yenyewe ilikua kila unapo fika mwezi wa February vijana wote walio fikisha umri wa kubaleghi wanajitolea kwa kasisi wao LUPERIUS wakitia majina yao kwenye bahati nasibu na wasichana pia wakifanya hivyo hivyo kuingiza majina yao kwenye bahati nasibu. Kisha baadae jina la mvulana lililoebu-ka, mshindi hufuatilizwa na jina la msichana alietoka mshindi kwenye wasichana wenzake na kulazimwishwa kuishi pamoja mvulana huyu na msichana huyu wakiwa wanazini pamoja kwa mda wa mwaka mmoja, ama mpaka urudi tena mwezi huu wa february wafanyiwe tena bahati nasibu nyengine wa angaliwe kama ita wabakisha waendelee kuishi pamoja kwa njia ya uzinifu au ita watenganisha kila mtu atafute mwenzake mwegine waanze kuishi pamoja wakiwa wanazini pamoja kupitisha kipindi kama hicho.
Kisha wa catholic walichukizwa na mila kama hiyo wa kaamua kumuondosha kasisi kama huyo kwa jina LUPERIUS Nakumuwe-ka kasisi mwegine kwa jina VALENTINE. Kasisi wakimape-nzi ambae pia yeye aliuliwa kwa kosa la kukhalifu amri ya mfalme wake CLAUDIUS. Mfalme huyu alipata tabu kubwa sana kwa wanajeshi wake waliyokua wame-oa kwa sababu walikua wakikataa kwenda vitani na kuwaacha wakezao majumbani. Ikabidi mfalme kama huyu akataze watu wake kuoana na kuwaruhusu waishi hivi hivi kwa njia ya uzinifu peke yake ili patokeapo amri ya watu kwenda vitani pasitokezee tena matatizo kama haya. Kasisi huyu wa valentine, akawa yeye yuwa fungisha watu ndoa za siri nje ya kanisa kwa ajili ya kutimiza maslaha yake na kutimiza moja wapo katika maju-kukumu yake kama kasisi au kama kiongozi wa kanisani. Mfalme wake alipo pata khabari kama hizi kuhusu kasisi huyu Aliamrisha ashikwe atiwe jela. Alipotiwa jela alikua ameshaanza mapenzi na msichana mmoja wa mkuu wa magereza. Ikabidi kabla ya kifo chake amuandikie msicha-na huyu Barua ampelekee Barua yenyewe ilikua imeandikwa na Damu akimuambia Barua hii yatoka kwa Valentine wako Aki-kusudia mpenzi wako na hi ndio sababu wakiristo ama makafiri wakawa siku hi 14 february wanavaa nguo nyekundu au kupe-lekeana mauwa mekundu (Red Rose). Sikwa sababu kua hawana nguo nyengine zaku vaa isipokua hizo wala hakuna mauwa mengine Dukani kununua kupelekeana Isi-pokua red rose laa bali ni kuiga na kunasibisha barua hii iliyo andikwa na Damu. Sasa ndugu muislamu siku kama hii ina mafu-ngamano gani na itikadi yako ya kiislamu mpaka ukawa unashere-hekea siku hi na kujifananisha nawao kuva nguo nyekudu au hujui Mtume S.A.W amesema mwenye kujifananisha nawatu fulani na yeye huwa kama wao kwa hivyo ndugu muis’lamu tusi-kubali kughuriwa nawao kwa tashwishi zao wanazo tushawishi nazo kwa sababu wao makafiri wanatamani sisi tutupe mismamo yetu yadini ili nasisi tuwe kama wao gora mmoja kama anavyo tu-elezea mwenyezi mungu nakutu fahamisha kwenye Qurani Akisema
ودوا لو تكفرون كما كفروا فتكونون سواء
kwamba makafiri wanatamani mno nyinyi wa is’lamu mukufuru kama wao walivyo kufuru mupate kua sawa sawa nawao ili mu siwe na misimamo yoyote yadini ye nu,
na sisi leo tumekua twa enda na wao popote wanapo enda na popote pale wa ingiyapo tuko nawao pasina ya ku jifahamu na ndipo bwana Mtume S.A.W Akabashiri habari hizi na kuziele-za kwenye hadithi Akisema
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :لتتبعن سنن الذين من كان قبلكم شبرا بشبر وذراعا بذراع حتى لو دخلوا في جحر ضب لتبعتموه {متفق عليه}
“Anasema Abu said Al-khudhriy (R.A) kuwa Mtume S.A.W Alise-ma yakua mutakuja kufuata nyendo zawalokuja kabla yenu shubiri kwa shubiri na mkono kwa mkono mpaka watakapo ingia kwenye shimo la kenge bado muta wafuata” Kwa haya machache tumuombe Allah atupe fahamu ya Dini yetu na athibitishe nyoyo zetu kwenye misimamo ndani ya Dini yetu na atuonyeshe haki kua ni jambo zuri na atuwezeshe kuifuata Na atuonyeshe batili kua nijambo baya Na atuwezeshe kuiyepuka.
Wa Billahi Tawfiq.
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM
ABUDUJANA
arms1423@hotmail.comرب اغفر لي ولوالدي، رب ارحمهما كما ربياني صغيرا
Usinisahau kwenye dua zako
INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM
اللهم اني أسألك علماً نافعاً و قلباً خاشعاً ولساناً ذاكراً
لا تنسوا إخوانكم في فلسطين والعراق وفي كل مكان بالدعاء
اللَّهُمَّ قَدْ تَدَاعَى اليَّهُودُ وَأَعْوَانُهُمْ عَلَى إِخْوانِنا الْمُسْلِمِينَ فِي فِلِسْطِينَ حَتَّى أَهْلَكُوا الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ، وَلاَ نَاصِرَ لَهُمْ مِنْ دُونِكَ، وَلاَ كَاشِفَ لُغُمَّتِهِمْ سِوَاكَ فَاجْعَلْ لَهُمْ مِنْ هَذَا الكَرْبِ فَرَجاً وَمَخْرَجاً وَأَيِّدْهُمْ بِنَصْرٍ مِنْ عِنْدِكَ وَادْحَرْ عَدُوَّهُمْ وَتَقَبَّلْ شُهَدَاءَهُمْ وَأَخْلِصْ نِيَّاتِهِمْ يَا رَبَّ العَالَمِينَ.