بسم الله الرحمن الرحيم
SUNNAH BAADAL ASRI
(HIZI NI HADITH KWA UFUPI TU )
مشروعية صلاة ركعتين بعد العصر (تذكير أهل السنة الحريصين على إحياء السنن و إماتة البدع
إن الحمد لله نحمده ونستعينه ونستغفره ، ونعوذ به من شرور أنفسنا وسيئات أعمالنا ، من يهده الله فلا مضل له ، ومن يضلل فلا هادي له ، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله صلى الله عليه وسلم .
أما بعد
كان لا يدع ركعتين قبل الفجر , و ركعتين بعد العصر "

ALIKUWA MTUME صلى الله عليه وسلم HAWACHI KUSWALI RAKAA MBILI KABLA YA FAJRI NA RAKAA MBILI BAADAL ASRI
لألباني في " السلسلة الصحيحة " 6 / 101
حدثتني الصديقة بنت الصديق حبيبة حبيب الله المبرأة : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يصلي ركعتين بعد العصر
IMEPOKEWA KUWA MTUME صلى الله عليه وسلمALIKUWA AKISWALI RAKAA MBILI BAADAL ASRI
و هذا إسناد صحيح أيضا على شرط الشيخين ,
و قد أخرجاه من طريق أخرى عن مسروق مقرونا مع الأسود بلفظ : " ما من يوم يأتي علي النبي صلى الله عليه وسلم إلا صلى بعد العصر ركعتين ": "
HAKUNA SIKU ANAYOKUJA MTUME ILLA HUSWALI RAKAA MBILI BAADAL ASRI
ركعتان لم يكن رسول الله صلى الله عليه وسلم يدعهما سرا و لا علانية : ركعتان قبل صلاة الصبح , و ركعتان بعد العصر " .
و في رواية بلفظ
RAKAA MBILI ALIKUWA MTUME HAZIWACHI KUZISWALI KWA SIRI AU KWA DHAHIRI RAKAA MBILI KABLA YA SWALA YA ASUBHI NA RAKAA MBILI BAADA YA SWALA YA AL ASRI
و هو مخرج في " الإرواء " ( 2 / 188 - 189 ) و الذي قبله في " صحيح أبي داود " ( 1160
.و هنا ينبغي أن نذكر أهل السنة الحريصين على إحياء السنن و إماتة البدع أن يصلوا هاتين الركعتين كلما صلوا العصر في وقتها المشروع , لقوله صلى الله عليه وسلم : " من سن في الإسلام سنة حسنة .. "
MPAKA HAPA NAPENDA KUWAKUMBUSHA KILA ALIE NA PUPA YA KUHUISHA SUNNAH YA MTUME صلى الله عليه وسلم KILA ANAPO MALIZA KUSWALI AL ASRI KATIKA WAKTI WAKE AZISWALI RAKAA MBILI HIZI
من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه

((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo)) (Muslim
. و بالله التوفيق
اللهم اني أسألك علماً نافعاً و قلباً خاشعاً ولساناً ذاكراً
بسم ا لله ا لر حمن الر حيم
KUAMRISHANA MEMA NA KUKATAZANA MAOVU NI LAZIMA KWA KILA MUISLAMU.
Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Allah anajua na nyinyi hamjui
Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Allah ni mpole, mwenye kurehemu
SI HIYARI KUKATAZA MAOVU NI LAZIMA
Asema Allah
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi . (Suratul Ahzab 36.)

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu basi akiondoe (akibadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani)) Muslim.
Na kwa kuacha amri hii ya kuamrishana mema ndio matatizo na kila aina ya madhara yanatufika na kubwa zaidi mwenye kuacha kazi hii atakuwa na LAANAA NA DUA ZAKE HAIKUBALIWI
Asema Allah“Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Awaonjeshe (adhabu ya) baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenyezi Mungu)”.Ar Rum – 41Ikiwa athari ya uharibifu inafika barani na baharini, basi bila shaka itakuwa wepesi zaidi kwa athari hiyo kumfikia mwenye kutenda maasi hayo pamoja na watu walio karibu naye.
Na akasema Subhanahu wa Taala;"Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake, ni marafiki wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema na kuyakataza yaliyo mabaya”.At - Tawba – 71
UNAPO NYAMAZIA UOVU UTAPATA ADHABU ALLAH
Ndani ya Qurani tukufu pia tunakuta mifano mingi inayotujulisha juu ya umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, na hapa nitautaja mfano mmoja wapo;Mayahudi katika dini yao walikatazwa siku ya Jumamosi wasijishughulishe na kazi yoyote ile isipokuwa wawe wanamuabudu Mwenyezi Mungu tu.Mwenyezi Mungu akataka kuwatia katika mtihani Mayahudi waliokuwa wakiishi katika kijiji kimoja cha wavuvi akajaalia iwe kila siku ya Jumamosi samaki wanakuja kwa wingi sana kuliko siku za kawaida.Wengine miongoni mwao wakashindwa kustahamili na wakaanza kuvua bila kuogopa, na wengine wakaona bora waipige chenga sheria hiyo ya Mwenyezi Mungu, wakawa siku ya Jumamosi wanakwenda kutega nyavu zao wapate kuwanasa samaki tu, lakini hawawachukuwi, mpaka siku ya Jumapili ndio wanakwenda kuwachukuwa.Baadhi ya watu wema miongoni mwao walikasirika tu, lakini hawakuwakataza wenzao wale waliokuwa wakivunja maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa kuipiga chenga siku hiyo ya Jumaamosi.Wengine wakawa wanawakataza wenzao, lakini wale watu wema walionyamaza wasikataze wakawa wanawaambia wenzao;“Kwa nini mnawaonya hali wao wanaelewa vizuri kuwa jambo hilo limekatazwa?”Basi ilipokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu wakapata adhabu wale waliokuwa wakiasi na pia wale walionyamaza wasiwakataze wenzao. Ama wale waliokuwa wakiwakataza wenzao, wao walisalimika na adhabu hiyo.Mwenyezi Mungu anasema:“Na waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari: (watu wa mji huo) walipokuwa wakivunja (Sheria ya) Jumaamosi (ambayo waliambiwa wasifanya kazi katika siku hiyo wafanye ibada tu. Na kazi yao ilikuwa uvuvi). Samaki wao walipowajia juu juu siku za Jumaamosi zao: na siku isiyokuwa Jumaamosi hawakuwa wakiwajia (hivyo). Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu ya kuasi kwao.Na (wakumbuke wakati) baadhi ya watu katika wao waliosema (kuwaonya walovunja hishima ya Jumaamosi kwa kuvua na hali yakuwa wamekatazwa waliposema): “Pana faida gani kuwaonya watu ambao Mwenyezi Mungu atawaua au atawaadhibu kwa adhabu kali (papa hapa)?” Wakasema: “Tupate kuwa na udhuru mbele ya Mola wenu (kuwa tumeonya lakini hatukusikilizwa) na huenda wakaogopa.”Basi walipoyapuuza waliyokuwa wakikumbushwa tuliwaokoa wale walokuwa wakikataza maovu, na tukawatesa wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa kuasi kwao.Na walipotakabari wasiache waliyokatazwa tuliwaambia: “Kuweni manyani madhalilifu”.Al Aaraf – 163-166Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema;“Na subirini, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanaofanya mema.Basi mbona hawakuwamo katika watu wa mbele kabla yenu watu wenye akili wenye kukataza uharibifu katika nchi? Isipokuwa wachache tu miongoni mwao ambao ndio tuliowaokoa.Na wale waliodhulumu (nafsi zao) walifuata waliyostareheshwa (maasi) na wakawa waovu”.Hud – 115-16Kwa ajili ya yote hayo Mwenyezi Mungu akatufaridhishia jukumu hili la kuamrisha mema na kukataza maovu na akawasifia Masahaba (RA) kuwa wao ni umma bora kupita umma zote kwa ajili ya kazi hii ngumu waliyoifanya kwa ukamilifu.
Mwenyezi Mungu anasema;“Nyinyi ndio umma bora kuliko uma zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) – mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu..”Aali Imran – 110Na akasema;“Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wakakataza maovu. Na hao ndio watakaotengenekewa”.Aali Imran – 104Na Mtume (SAW) akasema;"Maneno ya mwanadamu yote ni dhidi yake isipokuwa Kumtaja Mwenyezi Mungu au kuamrisha mema au kukataza maovu".Imepokelewa na Ibn Mardawea na kusimuliwa na Um Habiba (RA).WALLAHI MTAAMRISHA MEMAMwenyezi Mungu anasema;“Walilaaniwa wale walokufuru miongoni mwa wana wa Israili kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakipindukia mipaka (sana).Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya”.Al Maidah – 78-79Katika kuifasiri aya hii Mtume (SAW) alisema;“Mwanzo wa kuingia upotofu katika watu wa Bani Israil, ilikuwa mtu anapokutana na mwenzake (akimuona anafanya maasi) anamkataza kwa kumwambia;“Ewe mwenzangu muogope Mwenyezi Mungu na uache unayoyafanya kwani si halali kwako (kufanya hayo), kisha anaonana naye siku ya pili yake (mtu huyo) akiwa katika hali yake ile ile (akiwa anaendela na maasi yake), jambo hilo halimfanyi akaacha urafiki naye wala kuacha kula pamoja naye wala kuacha kukaa pamoja naye. Basi walipofanya vile, Mwenyezi Mungu akazipiganisha nyoyo zao baina yao”.Kisha Mtume (SAW) akaisoma aya hii;“Walilaaniwa wale walokufuru miongoni mwa wana wa Israili kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakipindukia mipaka (sana). Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya”.Kisha akasema;“La si hivyo Wallahi! (mkitaka mistake na nyinyi) Mtaamrisha mema na mtakataza maovu, kisha mtamshika mkono yule aliyejidhulumu, na kumuongoza katika haki na mtamfunga ndani ya haki, ama sivyo Mwenyezi Mungu atazipiganisha nyoyo zenu pia, kisha atakulaanini kama alivyowalani”.Attirmidhy - Abu Daud na wengine.