
السلام عليكم ورحمة الله وبركاته
وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا
((Na anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, Tutamuelekeza alikoelekea, na Tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa: 115
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangulizi wema mpaka Siku ya Mwisho.
WAKATI GANI WAKUKUMBATIANA WAKUPIGANA PAMBAJA (HUGING )
Leo imekuwa ni ada na desturi kila tunapokutana kukumbatiana(hug) na haswa baada ya swala ya Idd imekuwa ni kama salamu ya Idd, walakin hebu tuangalie jambo hili Maswahaba walikuwa wakilifanya vipi na sisi tuwaige kwani kuwaiga wao ndio kuongoka kwetu
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangulizi wema mpaka Siku ya Mwisho.
WAKATI GANI WAKUKUMBATIANA WAKUPIGANA PAMBAJA (HUGING )
Leo imekuwa ni ada na desturi kila tunapokutana kukumbatiana(hug) na haswa baada ya swala ya Idd imekuwa ni kama salamu ya Idd, walakin hebu tuangalie jambo hili Maswahaba walikuwa wakilifanya vipi na sisi tuwaige kwani kuwaiga wao ndio kuongoka kwetu
قال أنس رضي الله عنه : " كان أصحاب النبي صلى الله عليه وسلم إذا تلاقوا ؛ تصافحوا ، فإذا قدموا من سفرٍ ؛ تعانقوا " رواه الطبراني في الأوسط ،ورجاله رجال الصحيح
Walikuwa Masahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم wanapokutana hupeana mikono na wanapotoka safari hukumbatiana (hug)
كما قال المنذري (3/270) ،والهيثمي (8/36) . وروى البيهقي (7/100) بسند صحيح عن الشعبي : " كان أصحاب محمد صلى الله عليه وسلم إذا التقوا ؛ صافحوا ، فإذا قدموا من سفر ؛ عانق بعضهم بعضاً
Walikuwa Masahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم wanapokutana hupeana mikono na wanapotoka safari hukumbatiana (hug) Mmoja wao mwezie
". وروى البخاري في الأدب المفرد (970) ، وأحمد (3/495) عن جابر بن عبد الله قال : " بلغني حديث عن رجلٍ سمعه من رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فاشتريت بعيراً ، ثمّ شددتُ عليه رحلي ، فسرتُ إليه شهراً حتى قدمتُ عليه الشام ، فإذا عبد الله بن أنيس ، فقلت للبـواب : قل له : جابر على الباب . فقال : ابن عبد الله ؟ قلتُ : نعم . فخرج يطأ ثوبه فاعتنقني واعتنقته " الحديث . وإسناده حسن كما قال الحافظ ( 1/ 195
..Haifai Kutoa Mkono Kuamkiana Wanawake na Wanaume
عن معقل بن يسار يقول : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لئن يطعن في رأس أحدكم بمخيط من حديد خير له من أن يمس امرأة لا تحل له )) رواه الطبراني في " الكبير الحديث : قال الألباني عنه في " صحيح الجامع : صحيح
Imesimuliwa kutoka kwa Ma’qil ibn Yaassar ambaye amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake)) [At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuugusa mkono wa mwanamke bila ya kuwa na uhusiano wa kisheria naye (mahram yake), ataekewa kaa la moto kwenye kitanga chake cha mkono Siku ya Qiyaamah” (Fat-hul Qadiyr).
Mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikubali Bay‘ah ya wanawake kwa mdomo tu bila kushikana mikono. Hakika hakugusa mkono wa mwanamke ambaye si mkewe (al-Bukhaariy).
Ni wazi kuwa katika Baiyah ya kwanza, waliyomuahidi kwayo Ma-Answaar waliokuwa wanaume watupu inajulikana katika Siyrah kama Bay‘ah ya kike kwani walitakiwa waahidi kama yale ya wanawake waliokuja baadaye, tofauti yake ni kuwa wanaume walimpatia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mikono yao. Allaah Anasema:
“Ewe Nabii! Wanapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Allaah na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaozusha tu wenyewe baina ya mikono na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana ahadi nao na uwatakie maghfira kwa Allaah. hakika Allaah ni Mwingi wa maghfira, Mwingi wa rehema” (60: 12).
Akasema ‘Aaishah: yeyote katika waumini wanawake aliyekubali hayo na akapasi walipokubali Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: ((Nendeni kwani mmetimiza kiapo cha utiifu)) Hapana! Naapa kwa Allaah, mkono wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haukugusa mkono wa mwanamke yeyote bali walitoa viapo vyao vya utiifu kwa maneno pekee”. Kisha ‘Aaishah akasema: “Naapa kwa Allaah, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokea viapo vya utiifu kwa njia Aliyoitolea sheria Allaah na mkono wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haujapata kugusa mkono wa mwanamke yeyote. Alipofungamana nao viapo vya utiifu alisema: ((Nimekubali kiapo chako cha utiifu [kwa matamshi])) [Muslim]
Vile vile:
عن أميمة ابنة رقيقة قالت : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إني لا أصافح النساء)) رواه النسائي وابن ماجه وصححه الألباني " صحيح الجامع
Imetoka kwa Umaymah bint Raqiyqah ambaye amesema: “Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mimi sisalimiani na wanawake kwa kupeana nao mkono) [An-Nasaaiy, Ibn Maajah na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jaami’]
Tunatumai kuwa dalili hizo zitakuwa ni mafunzo miongoni mwa ndugu zetu ambao wana tabia hii ya kuamkiana kwa mikono na wanaume wasio mahram wao ili wabakie katika radhi za Mola wao na pia kuepukana na madhara yake.
((وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا))
((Na anachokupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho)) [Al-Hashr: 7]
Wa Allaahu A'alam
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْكSubhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM
IMETAYARISHWA NA ABUDUJANA arms1423@hotmail.com
Usinisahau kwenye dua zako
INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM
No comments:
Post a Comment