Tuesday, July 14, 2009


بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

HAKUNA SAUM YAITWA SAUM YA MIIRAJ
Tukio la Miiraj nitukio Asema Allah Alietakasika na akatukuka :-


سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
((Ametakasika Aliyemchukua mja Wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali,
ambao Tumevibariki vilivyouzunguka, ili Tumuonyeshe baadhi ya Ishara Zetu. Hakika Yeye ni Mwenye
kusikia na Mwenye kuona))
[Al-Israa: 1]
na ni katika aqida yetu kuiamini hii safari Asema Imaam Abu Ja’afar at-Tahaawi katika kitabu chake
‘Aqeedatu at-Tahaawiyah
Mi'raaj ni kweli, na mtume Salallahu Alaihi Wasallam alichukuluwa katika safari ya al-Israa kiwiliwili chake, akiwa macho na wala sio usingizini hadi mbinguni kisha akapandishwa hadi sehemu aliyopenda Allah, na Allah akamuadhimu Kwake vile Alivyopenda. Na akamfunulia yale aliyotaka kumfunulia (Moyo haukusema uwongo uliyo yaona) [An-Najm:11]. Basi tunamwomba Allah amuenue daraja na amfikishie Rehma na Amani kesho siku ya akhera na kabla ya hapo
LINI LILITOKEA TUKIO HILI:-
Ama kuhusu usiku wenyewe wa tukio hili la Israa na Mi'iraaj hakuna Hadiyth Swahiyh inayoelezea kuwa ilikuwa katika mwezi wa Rajab au tarehe 27 ya mwezi huu wa Rajab kama wengi wanavyodhania. Usimulizi wowote unaotaja mwezi au tarehe ya tukio hili umekosa dalili Swahiyh kama wasemavyo Maulaama wa Hadiyth. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa hikma Yake Amewafanya watu wasahau siku hii. Hata kama ingelikuwa hiyo siku imetajwa katika dalili basi isingeliruhusiwa Muislamu kuipwekesha kwa kufanya ibada fulani au kusherehekea. Hii kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala Maswahaba zake hawakufanya hivyo. Na ingelikuwa kuipwekesha ni amri iliyo katika Dini yetu basi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) angelitoa mafunzo kwa Ummah wake kwa kauli au vitendo. Na ingelikuwa imefanyika zama zake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi bila shaka ingelijulikana na usimulizi ungelitufikia kwa isnaad Swahiyh kama tulivyopata mafunzo mengineyo ya uhakika

VILE VILE HAKUNA SAUM YA MWEZI WA RAJAB SEMBUSE SAUM YA MIIRAJ


kunapendekezwa mtu kufanya ibada aina yoyote inayoambatana na sheria kwa wingi, katika miezi mitukufu ambao Rajab ni miongoni mwao
Asema Allah:-
( إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِنْدَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْراً فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنْفُسَكُمْ ) التوبة/36 , والأشهر الحرم هي : رجب , وذو العقدة , وذو الحجة , والمحرم .
Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu.
Hakika hisabu ya miezi ya kuandama ni miezi kumi na mbili, kwa hukumu na kudra ya Mwenyezi Mungu, na ndivyo alivyo ibainisha katika vitabu vyake tangu kuanza ulimwengu. Na katika hii miezi thinaashara ipo mine imekatazwa kupigana vita ndani yake, nayo:-Mwezi wa Rajab, Alqa'ada (Mfungo Pili), Alhijja (Mfungo Tatu), na Almuharram (Mfungo Nne). Na huku kuitukuza miezi hii mine na kuharimisha kupigana vita ndani yake ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka, ambayo haibadiliki wala haina mageuzo. Basi msijidhulumu nafsi zenu kwa kuhalalisha vita katika miezi hii, au mkaacha kujilinda adui akikupigeni. Na enyi Waumini! Piganeni na washirikina bila ya kumbagua yeyote kati yao, kama wanavyo kupigeni nyinyi nyote. Na kuweni na yakini kuwa Mwenyezi Mungu atawanusuru wanao mcha, na wakashika amri zake, na wakaepuka anayo yakataza.
WALAKIN HAKUNA MAKHSUS ZA IBADA MAALIM ZA MWEZI WA RAJAB HASWA SAUM

عن خرشة قال: رأيت عمر بن الخطاب يضرب أكف الرجال في صوم رجب حتى يضعونها في الطعام ويقول رجب وما رجب إنما رجب شهر كان يعظمه أهل الجاهلية فلما جاء الإسلام ترك مجمع الزوائد : 3/194
“Nilimuona Umar akiichapa mikono ya wale waliyokuwa wamefunga mwezi wa Rajab mpaka walipofungulia, na alikuwa akisema huu ni mwezi uliyokuwa ukiheshimiwa sana wakati wa jahiliya. (kabla ya Uislamu) Na ulipokuja Uislam Ukaachwa. (Majma'u az-Zawaaid Mj. 3 Uk. 194)(al-Irwaa’, 957; Shaykh Al-Albaaniy kasema ni Sahihi).

قال شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله في "مجموع الفتاوى" (25/290) :
" وأما صوم رجب بخصوصه فأحاديثه كلها ضعيفة ، بل موضوعة ، لا يعتمد أهل العلم على شيء منها ، وليست من الضعيف الذي يروى في الفضائل ، بل عامتها من الموضوعات المكذوبات

Anasema sheikh Islam Ibnu Taymiyyah :-
Hakika kuifanya saum makhsus kwa mwezi wa Rajab hadith zote ni dhaifu, bali ni maudhui(amesingiziwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)hawazitegemei maulamaa hadithi hizo wala si dhaifu ambazo hutegemewa katika fadhail walakin karibu zote ni maudhui na za urongo....."
مجموع الفتاوى" (25/290)

قال ابن القيم رحمه الله :
" كل حديث في ذكر صيام رجب وصلاة بعض الليالي فيه فهو كذب مفترى " انتهى من "المنار المنيف" (ص96)


Vilevile anasema Sheikh Al Allama Ibnul Qayyim :-
Kila hadith iliotaja kufunga mwezi wa Rajab na kuswali katika baadhi ya usiku wake ni za uorongo na kuzuliwa ("المنار المنيف" (ص96))

وقال الحافظ ابن حجر في "تبيين العجب" (ص11) :
" لم يرد في فضل شهر رجب , ولا في صيامه ولا صيام شيء منه معين , ولا في قيام ليلة مخصوصة فيه حديث صحيح يصلح للحجة " انتهى
.
Na amesema Al Hafidh Ibnul Hajar :-
Haikupokewa katika Fadhla za Rajab wala katika kufunga kitu chochote makhsus(special) wala katika kuswali usiku katika usiku wake swala makhsus katika hadith saheeh ambayo itakuwa ni hoja .."تبيين العجب" (ص11)


وقال الشيخ سيد سابق رحمه الله في "فقه السنة" (1/383) :
" وصيام رجب ليس له فضل زائد على غيره من الشهور , إلا أنه من الأشهر الحرم , ولم يرد في السنة الصحيحة أن للصيام فضيلة بخصوصه , وأن ما جاء في ذلك مما لا ينتهض للاحتجاج به
"
ِAnasema Sheikh Sayyid sabiq :-
Na kufunga Rajab hakuna fadhla zaidi na miezi mengineo, ispokuwa ni mwezi miongoni mwa miezi mitukufu, wala haikupokewa katika hadith sahih ya kwamba katika kufunga rajab kuna fadhla makhsus,na yaliopokewa kwa haya siyakutegemewa kutolewa hoja.فقه السنة" (1/383)

وسئل الشيخ ابن عثيمين رحمه الله عن صيام يوم السابع والعشرين من رجب وقيام ليلته .
فأجاب :
" صيام اليوم السابع العشرين من رجب وقيام ليلته وتخصيص ذلك بدعة , وكل بدعة ضلالة " انتهى .


Na akaulizwa Sheikh Ibnu Uthaimeen Allah amrehemu kuhusu kufunga tarehe 27 ya Mwezi wa Rajab (ijulikanayo kama saum ya Miiraj).
Akajibu:- Kufunga siku ya 27 mwezi wa Rajab nakuhusisha usiku wake kuswali , Ni Bid'a na kila bid'a ni UPOTEVU."مجموع فتاوى ابن عثيمين" (20/
Ewe Muislam zingatia haya:-
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah: 3]
Hivyo mwenye kufanya kitendo ambacho hakimo katika Dini yetu itakuwa ni kupoteza muda wake kwa ibada isiyo na thamani kama tulivyoonywa:
من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) Al-Bukhaariy

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika khutbah yake mwisho kwenye Hijjatul-widaa' alisema:
يا أيها الناس، ما من شيء يقربكم إلى الجنة ويباعدكم من النار إلا وقد أمرتكم به، وما من شيء يقربكم من النار ويباعدكم من الجنة إلا وقد نهيتكم عنه
((Enyi watu, hakuna jambo lolote ambalo litakukurubisheni na Pepo na kukuepusheni na moto ila nimekuamrisheni nalo. Na hakuna jambo lolote litakalokukurubisheni na moto au kukuepusheni na Pepo ila nimekukatazeni nalo))


Kwa nini Muislamu ajitakie mashaka zaidi ya kufanya ‘Ibaadah isiyokuwa na dalili? Kwa nini kwanza asitimize hizo ambazo tayari dalili zake ziko wazi? Kama Muislamu anapenda sana ‘Ibaadah ya kufunga basi afunge Swawm ya Daawuud lakini wangapi wanaoweza kufanya ‘Ibaadah hiyo?
Juu ya hivyo kufuata bid'ah (uzushi) ni upotofu na kujitakia mtu mwenyewe kuwa na makazi mabaya siku ya Qiyaamah:
إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمدصلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكلضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allaah (Qur-aan) na uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika Dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni))[Muslim katika Swahiyh yake]
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM

INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM
Imetayarishwa na
Arms1423@hotmail.com.

No comments:

Post a Comment