Saturday, August 1, 2009

NUSU YA SHAABAN




بسم الله الرحمن الرحيم

NUSU SHAABAN

{ وكذلك نفصل الآيات ولتستبين سبل المجرمين } [ الأنعام : 55

Na ndio hivi tunavyo zieleza Ishara ili ibainike njia ya wakosefu
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah: 3]

((وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا))
((Na anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, Tutamuelekeza alikoelekea, na Tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa: 115

HAYA NDIO YALIOPOKEWA KUHUSU NUSFU SHAABAN
عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: إن الله ليطلع في ليلة النصف من شعبان فيغفر لجميع خلقه إلا لمشرك أو مشاحن )) رواه ابن ماجة وحسنه الألباني في السلسلة الصحيحة
((Imetoka kwa Abu Muusa Al-Ash'ariy رضي الله عنه kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema: Hutokea Allaah سبحانه وتعالىKatika usiku wa 15 wa Sha'abaan, na Huwasamehe wote isipokuwa Washirikina au mzushi )) Ibn Maajah na imesemwa kuwa ni Hadiyth Hasan na Shaykh Al-Albaaniy.

قال الشيخ الألباني رحمه الله
في تخريج إصلاح المساجد للقاسمي (ص88)
لا يلزم من ثبوت هذا الحديث اتخاذ هذه الليلة موسماً يجتمع الناس فيها
ويفعلون فيها من البدع
Amesema Sheikh Albaani (Rehma za MwenyeziMungu zimfikie) hailazimu kwa kuthibiti hadithi hii kuufanya usiku huo ni msimu ambao watu wana kusanyika ndani yake na kufanya ya uzushi
,kisha kama ilivyodhahiri hakuna katika hadithi hiyo ishara ya watu kufanya ibada usiku wake au kufunga mchana wake,na qauli ya wanavyuoni wengi ni kwamba kukusanyika katika swala hili ni kwa sababu haikuswihi hadithi katika usiku huo kutokana na Mtume (Rehma na amani zimfikie) wala hakutamka kua watu wa swali katika usiku huo na kuwasha moto, na mambo waliyo yazusha wenye kuchezea sheria ya Mtume (Rehma na amani zimfikie)
.


Kuufanya makhsus usiku wa nusfu shaaban kwa kusmama usiku kuswali au kufanya ibada nyenginezo sio sunnah bali ni bida’a

Amesema sheikh ibnu uthaimeen:-

أن ليلة النصف من شعبان كغيرها من الليالي، لا تخص بقيام, ولا يوم النصف بصيام
لكن من كان يقوم كل ليلة, فلا نقول لا تقم ليلة النصف ومن كان يصوم أيام البيض لا نقول لا تصم أيام النصف إنما نقول: لا تخص ليلها بقيام ولا نهارها بصيام

Ya kwamba usiku wa nusu ya shaaban ni sawa kama usiku mwengine, musiufanye makhsus kwa kuswali usiku na kufunga mchana wake,walakin yule ambae yuwaswali kila usiku hatumkatazi kuswali usiku huu na ambae yuwafunga ayyam ala beidh hatumkatazi walakin twasema haifai kuufanya usiku na mchana wa nusu ya shaaban makhsus kwa kufunga au kusmama usiku.


Na amesema Mwanachuoni wa Al Jazira Sheikh Ibn Baaz katika mwisho wa (Bah’thi) utafiti wake “na kutokana na aya na hadithi na maneno ya wanavyuoni yaliotangulia hubainika kwa mwenye kutaka haki kwamba hukusanyika katika usiku wa nusu ya Shaaban kwa kuswali au kwa ibada nyengine na kuuhusu mchana wake kwa kufunga ni uzushi wenye kukatazwa na wanavyuoni wengi na jambo hilo halina dalili yoyote katika sheria takatifu, tena jambo hilo limezuka katika uislamu baada ya zama za maswahahaba….(”At – Tahdhiru Minal Bid’aah ya Ibn Baaz uk 27)

AMA KUHUSU KUSOMA YASIIN TATU
قراءة يس ثلاث مرات، المرة الاولى بنية طول العمر ، والمرة الثانية بنية دفع البلاء ، والمرة الثلاثة بنية الرزق .

Yaseen ya kwanza kwa nia kuwa na umri mrefu , yapili kwa kuondoa balaa naya tatu kwa kukunduliwa kwa rizki na kila baada ya yasinn kusoma dua hii:-:
اللهم يا ذا المن لا يمن عليه احد يا ذا الجلال والإكرام يا ذا الطول والأنعام…………………،

Haya hayapo katika mafundisho wa dini yetu kama yapo yangetufikia walakin Jee Mtume (Rehma na amani zimfikie) aliyasoma haya, au Maswahaba au Maimamu wanne waliyafanya haya??????????


Memeyapata wapi???
قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِنْ كُنتُمْ صَادِقِينَ
Sema: Leteni ushahidi wenu kama nyinyi ni wasema kweli SURA AL- BAQARA 111
Kama hamuna dalili basi Allah awaambia:-
قُلْ أَتُعَلِّمُونَ اللَّهَ بِدِينِكُمْ
Sema: Ati ndio mnamfundisha Mwenyezi Mungu Dini yenu??
16). (SURAT AL H'UJURAAT
Mtume (Rehma na amani zimfikie) asema
من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) Al-Bukhaariy
ترجو النجاة ولم تسلك مسالكها: إن السفينة لا تجرى على اليبس.

“Unatarajia kuokoka (kufaulu) bila ya kupita katika njia zake (Elewa kwamba) jahazi haiwezi kwenda kwenye nchi kavu.”

Mshairi mwengine anasema:

وإن أتيت الأمر من غير بابه: ضللت وإن تدخل من الباب تهتد.

“Ukiliendea jambo (ukitaka kulifanya jambo) bila ya kupita katika njia zake utapotea (na kuwapoteza wenzako). Na ukiliingia jambo katika njia zake utaongoka (na utaongoza wenzako).”


يا أيها الذين آمنـوا إن كـثـيراً من الأحـبار والرهبــان ليأكلون أموال الناس بالباطل ويصـدون عن سبـيـل الله } [ التوبة : 34

. Enyi mlio amini! Hakika wengi katika makuhani na wamonaki wanakula mali za watu kwa baat'ili na wanazuilia Njia ya Mwenyezi Mungu.

Allah Asema:-
((اتَّبِعُواْ مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلاَ تَتَّبِعُواْ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاء))
((Fuateni mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au walinzi wengine badala yake

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika khutbah yake mwisho kwenye Hijjatul-widaa' alisema:
يا أيها الناس، ما من شيء يقربكم إلى الجنة ويباعدكم من النار إلا وقد أمرتكم به، وما من شيء يقربكم من النار ويباعدكم من الجنة إلا وقد نهيتكم عنه
((Enyi watu, hakuna jambo lolote ambalo litakukurubisheni na Pepo na kukuepusheni na moto ila nimekuamrisheni nalo. Na hakuna jambo lolote litakalokukurubisheni na moto au kukuepusheni na Pepo ila nimekukatazeni nalo))
إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمدصلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكلضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allaah (Qur-aan) na uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika Dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni))[Muslim katika Swahiyh yake

Na Amesema Allah -azza wajalla-:
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ آمِنُواْ آَمَا آمَنَ النَّاسُ قَالُواْ أَنُؤْمِنُ آَمَا آمَنَ السُّفَهَاء أَلا إِنَّهُمْ هُمُ السُّفَهَاء وَلَكِن لاَّ يَعْلَمُون

“Na wanapoambiwa:aminini KAMA WALIVYOAMINI WATU wanasema;
Tuamini kama walivyoamini wapumbavu?...”.
Suratul-Baqarah aya ya 13.

Imepokewa kutoka kwa Ibnu Mas’oud na Ibn Abbaas kwamba
wamesema: “Watu waliokusudiwa hapa ni maswahaba”.
Tazama tafsiri al-Durrul-Manthuur juzuu ya 1 ukurasa 70-71.

Na amesema tena Allah:
فَإِنْ آمَنُواْ بِمِثْلِ مَا آمَنتُم بِهِ فَقَدِ اهْتَدَواْ وَّإِن تَوَلَّوْاْ فَإِنَّمَا هُمْ فِي شِقَاقٍ فَسَيَكْفِيكَهُمُ اللّهُ وَهُوَ السَّمِيعُ
الْعَلِيمُ البقرة 137
“Basi wakiamini KAMA MLIVYOAMINI NYINYI (maswahaba) basi
watakuwa wameongoka.Na wakikengeuka basi wao wamo katika
upinzani”.
Suratul Baqarah aya ya 137.


Amesema Allah:
والسابقون الأولون من المهاجرين والأنصار والذين اتبعوهم بإحسان رضي الله عنهم ورضوا
عنه...الآية
“Na wale waliotangulia, wakwanza katika Muhajirina na Answaari,nawale waliowafuata kwa wema, Allah ameridhika nao, na waowameridhika naye....”.
Suratut Tawba aya ya 100.
Kwa mujibu wa aya hizo zote tulizozitaja, tunatakiwa waislamu wotekuamini kama walivyoamini maswahaba wa Mtume Muhammad -swalla llaahu alayhi wasallam- pamoja na kuifuata njia waliyoipita. Na kama imani zetu zitatofautiana na imani zao na njia yetu
ikitofautiana na njia yao, basi tutakuwa ndani ya mashaka makubwamno na upotevu uliowazi kama zilivyoeleza aya tulizozitaja.
Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema

((فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))
((Basi na watahadhari wanaokhalifu amri yake, usije ukawapata msiba au ikawapata adhabu iumizayo))

سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك





Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka



Tuesday, July 14, 2009


بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

HAKUNA SAUM YAITWA SAUM YA MIIRAJ
Tukio la Miiraj nitukio Asema Allah Alietakasika na akatukuka :-


سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ لِنُرِيَهُ مِنْ آيَاتِنَا إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ البَصِيرُ
((Ametakasika Aliyemchukua mja Wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali,
ambao Tumevibariki vilivyouzunguka, ili Tumuonyeshe baadhi ya Ishara Zetu. Hakika Yeye ni Mwenye
kusikia na Mwenye kuona))
[Al-Israa: 1]
na ni katika aqida yetu kuiamini hii safari Asema Imaam Abu Ja’afar at-Tahaawi katika kitabu chake
‘Aqeedatu at-Tahaawiyah
Mi'raaj ni kweli, na mtume Salallahu Alaihi Wasallam alichukuluwa katika safari ya al-Israa kiwiliwili chake, akiwa macho na wala sio usingizini hadi mbinguni kisha akapandishwa hadi sehemu aliyopenda Allah, na Allah akamuadhimu Kwake vile Alivyopenda. Na akamfunulia yale aliyotaka kumfunulia (Moyo haukusema uwongo uliyo yaona) [An-Najm:11]. Basi tunamwomba Allah amuenue daraja na amfikishie Rehma na Amani kesho siku ya akhera na kabla ya hapo
LINI LILITOKEA TUKIO HILI:-
Ama kuhusu usiku wenyewe wa tukio hili la Israa na Mi'iraaj hakuna Hadiyth Swahiyh inayoelezea kuwa ilikuwa katika mwezi wa Rajab au tarehe 27 ya mwezi huu wa Rajab kama wengi wanavyodhania. Usimulizi wowote unaotaja mwezi au tarehe ya tukio hili umekosa dalili Swahiyh kama wasemavyo Maulaama wa Hadiyth. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa hikma Yake Amewafanya watu wasahau siku hii. Hata kama ingelikuwa hiyo siku imetajwa katika dalili basi isingeliruhusiwa Muislamu kuipwekesha kwa kufanya ibada fulani au kusherehekea. Hii kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala Maswahaba zake hawakufanya hivyo. Na ingelikuwa kuipwekesha ni amri iliyo katika Dini yetu basi Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) angelitoa mafunzo kwa Ummah wake kwa kauli au vitendo. Na ingelikuwa imefanyika zama zake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) basi bila shaka ingelijulikana na usimulizi ungelitufikia kwa isnaad Swahiyh kama tulivyopata mafunzo mengineyo ya uhakika

VILE VILE HAKUNA SAUM YA MWEZI WA RAJAB SEMBUSE SAUM YA MIIRAJ


kunapendekezwa mtu kufanya ibada aina yoyote inayoambatana na sheria kwa wingi, katika miezi mitukufu ambao Rajab ni miongoni mwao
Asema Allah:-
( إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِنْدَ اللَّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْراً فِي كِتَابِ اللَّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنْفُسَكُمْ ) التوبة/36 , والأشهر الحرم هي : رجب , وذو العقدة , وذو الحجة , والمحرم .
Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu.
Hakika hisabu ya miezi ya kuandama ni miezi kumi na mbili, kwa hukumu na kudra ya Mwenyezi Mungu, na ndivyo alivyo ibainisha katika vitabu vyake tangu kuanza ulimwengu. Na katika hii miezi thinaashara ipo mine imekatazwa kupigana vita ndani yake, nayo:-Mwezi wa Rajab, Alqa'ada (Mfungo Pili), Alhijja (Mfungo Tatu), na Almuharram (Mfungo Nne). Na huku kuitukuza miezi hii mine na kuharimisha kupigana vita ndani yake ndiyo Dini ya Mwenyezi Mungu Iliyo Nyooka, ambayo haibadiliki wala haina mageuzo. Basi msijidhulumu nafsi zenu kwa kuhalalisha vita katika miezi hii, au mkaacha kujilinda adui akikupigeni. Na enyi Waumini! Piganeni na washirikina bila ya kumbagua yeyote kati yao, kama wanavyo kupigeni nyinyi nyote. Na kuweni na yakini kuwa Mwenyezi Mungu atawanusuru wanao mcha, na wakashika amri zake, na wakaepuka anayo yakataza.
WALAKIN HAKUNA MAKHSUS ZA IBADA MAALIM ZA MWEZI WA RAJAB HASWA SAUM

عن خرشة قال: رأيت عمر بن الخطاب يضرب أكف الرجال في صوم رجب حتى يضعونها في الطعام ويقول رجب وما رجب إنما رجب شهر كان يعظمه أهل الجاهلية فلما جاء الإسلام ترك مجمع الزوائد : 3/194
“Nilimuona Umar akiichapa mikono ya wale waliyokuwa wamefunga mwezi wa Rajab mpaka walipofungulia, na alikuwa akisema huu ni mwezi uliyokuwa ukiheshimiwa sana wakati wa jahiliya. (kabla ya Uislamu) Na ulipokuja Uislam Ukaachwa. (Majma'u az-Zawaaid Mj. 3 Uk. 194)(al-Irwaa’, 957; Shaykh Al-Albaaniy kasema ni Sahihi).

قال شيخ الإسلام ابن تيمية رحمه الله في "مجموع الفتاوى" (25/290) :
" وأما صوم رجب بخصوصه فأحاديثه كلها ضعيفة ، بل موضوعة ، لا يعتمد أهل العلم على شيء منها ، وليست من الضعيف الذي يروى في الفضائل ، بل عامتها من الموضوعات المكذوبات

Anasema sheikh Islam Ibnu Taymiyyah :-
Hakika kuifanya saum makhsus kwa mwezi wa Rajab hadith zote ni dhaifu, bali ni maudhui(amesingiziwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)hawazitegemei maulamaa hadithi hizo wala si dhaifu ambazo hutegemewa katika fadhail walakin karibu zote ni maudhui na za urongo....."
مجموع الفتاوى" (25/290)

قال ابن القيم رحمه الله :
" كل حديث في ذكر صيام رجب وصلاة بعض الليالي فيه فهو كذب مفترى " انتهى من "المنار المنيف" (ص96)


Vilevile anasema Sheikh Al Allama Ibnul Qayyim :-
Kila hadith iliotaja kufunga mwezi wa Rajab na kuswali katika baadhi ya usiku wake ni za uorongo na kuzuliwa ("المنار المنيف" (ص96))

وقال الحافظ ابن حجر في "تبيين العجب" (ص11) :
" لم يرد في فضل شهر رجب , ولا في صيامه ولا صيام شيء منه معين , ولا في قيام ليلة مخصوصة فيه حديث صحيح يصلح للحجة " انتهى
.
Na amesema Al Hafidh Ibnul Hajar :-
Haikupokewa katika Fadhla za Rajab wala katika kufunga kitu chochote makhsus(special) wala katika kuswali usiku katika usiku wake swala makhsus katika hadith saheeh ambayo itakuwa ni hoja .."تبيين العجب" (ص11)


وقال الشيخ سيد سابق رحمه الله في "فقه السنة" (1/383) :
" وصيام رجب ليس له فضل زائد على غيره من الشهور , إلا أنه من الأشهر الحرم , ولم يرد في السنة الصحيحة أن للصيام فضيلة بخصوصه , وأن ما جاء في ذلك مما لا ينتهض للاحتجاج به
"
ِAnasema Sheikh Sayyid sabiq :-
Na kufunga Rajab hakuna fadhla zaidi na miezi mengineo, ispokuwa ni mwezi miongoni mwa miezi mitukufu, wala haikupokewa katika hadith sahih ya kwamba katika kufunga rajab kuna fadhla makhsus,na yaliopokewa kwa haya siyakutegemewa kutolewa hoja.فقه السنة" (1/383)

وسئل الشيخ ابن عثيمين رحمه الله عن صيام يوم السابع والعشرين من رجب وقيام ليلته .
فأجاب :
" صيام اليوم السابع العشرين من رجب وقيام ليلته وتخصيص ذلك بدعة , وكل بدعة ضلالة " انتهى .


Na akaulizwa Sheikh Ibnu Uthaimeen Allah amrehemu kuhusu kufunga tarehe 27 ya Mwezi wa Rajab (ijulikanayo kama saum ya Miiraj).
Akajibu:- Kufunga siku ya 27 mwezi wa Rajab nakuhusisha usiku wake kuswali , Ni Bid'a na kila bid'a ni UPOTEVU."مجموع فتاوى ابن عثيمين" (20/
Ewe Muislam zingatia haya:-
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الإِسْلاَمَ دِينً
((Leo Nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni Neema Yangu, na Nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini)) [Al-Maaidah: 3]
Hivyo mwenye kufanya kitendo ambacho hakimo katika Dini yetu itakuwa ni kupoteza muda wake kwa ibada isiyo na thamani kama tulivyoonywa:
من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu (katika dini yetu) basi kitarudishwa)) Al-Bukhaariy

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika khutbah yake mwisho kwenye Hijjatul-widaa' alisema:
يا أيها الناس، ما من شيء يقربكم إلى الجنة ويباعدكم من النار إلا وقد أمرتكم به، وما من شيء يقربكم من النار ويباعدكم من الجنة إلا وقد نهيتكم عنه
((Enyi watu, hakuna jambo lolote ambalo litakukurubisheni na Pepo na kukuepusheni na moto ila nimekuamrisheni nalo. Na hakuna jambo lolote litakalokukurubisheni na moto au kukuepusheni na Pepo ila nimekukatazeni nalo))


Kwa nini Muislamu ajitakie mashaka zaidi ya kufanya ‘Ibaadah isiyokuwa na dalili? Kwa nini kwanza asitimize hizo ambazo tayari dalili zake ziko wazi? Kama Muislamu anapenda sana ‘Ibaadah ya kufunga basi afunge Swawm ya Daawuud lakini wangapi wanaoweza kufanya ‘Ibaadah hiyo?
Juu ya hivyo kufuata bid'ah (uzushi) ni upotofu na kujitakia mtu mwenyewe kuwa na makazi mabaya siku ya Qiyaamah:
إن خير الكلام كلام الله وخير الهدي هدي محمدصلى الله علي وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة وكلضلالة في النار)) أخرجه مسلم في صحيحه
((Maneno bora ni kitabu cha Allaah (Qur-aan) na uongofu mbora kabisa ni uongofu wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi, na kila jambo jipya (katika Dini) ni bid'ah (uzushi) na kila bid'ah ni motoni))[Muslim katika Swahiyh yake]
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك
Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM

INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM
Imetayarishwa na
Arms1423@hotmail.com.

Wednesday, July 8, 2009

WAKATI GANI WAKUKUMBATIANA WAKUPIGANA PAMBAJA (HUGING – عانق إ)Haifai Kutoa Mkono Kuamkiana Wanawake na Wanaume

BISMILLAHI RAHMANI RAHEEM



السلام عليكم ورحمة الله وبركاته

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَى وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّى وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ وَسَاءتْ مَصِيرًا
((Na anayempinga Mtume baada ya kumdhihirikia uongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, Tutamuelekeza alikoelekea, na Tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu)) [An-Nisaa: 115

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangulizi wema mpaka Siku ya Mwisho.

WAKATI GANI WAKUKUMBATIANA WAKUPIGANA PAMBAJA (HUGING )

Leo imekuwa ni ada na desturi kila tunapokutana kukumbatiana(hug) na haswa baada ya swala ya Idd imekuwa ni kama salamu ya Idd, walakin hebu tuangalie jambo hili Maswahaba walikuwa wakilifanya vipi na sisi tuwaige kwani kuwaiga wao ndio kuongoka kwetu

قال أنس رضي الله عنه : " كان أصحاب النبي صلى الله عليه وسلم إذا تلاقوا ؛ تصافحوا ، فإذا قدموا من سفرٍ ؛ تعانقوا " رواه الطبراني في الأوسط ،ورجاله رجال الصحيح
Walikuwa Masahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم wanapokutana hupeana mikono na wanapotoka safari hukumbatiana (hug)
كما قال المنذري (3/270) ،والهيثمي (8/36) . وروى البيهقي (7/100) بسند صحيح عن الشعبي : " كان أصحاب محمد صلى الله عليه وسلم إذا التقوا ؛ صافحوا ، فإذا قدموا من سفر ؛ عانق بعضهم بعضاً
Walikuwa Masahaba wa Mtume صلى الله عليه وسلم wanapokutana hupeana mikono na wanapotoka safari hukumbatiana (hug) Mmoja wao mwezie


". وروى البخاري في الأدب المفرد (970) ، وأحمد (3/495) عن جابر بن عبد الله قال : " بلغني حديث عن رجلٍ سمعه من رسول الله صلى الله عليه وسلم ، فاشتريت بعيراً ، ثمّ شددتُ عليه رحلي ، فسرتُ إليه شهراً حتى قدمتُ عليه الشام ، فإذا عبد الله بن أنيس ، فقلت للبـواب : قل له : جابر على الباب . فقال : ابن عبد الله ؟ قلتُ : نعم . فخرج يطأ ثوبه فاعتنقني واعتنقته " الحديث . وإسناده حسن كما قال الحافظ ( 1/ 195
..Haifai Kutoa Mkono Kuamkiana Wanawake na Wanaume
عن معقل بن يسار يقول : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( لئن يطعن في رأس أحدكم بمخيط من حديد خير له من أن يمس امرأة لا تحل له )) رواه الطبراني في " الكبير الحديث : قال الألباني عنه في " صحيح الجامع : صحيح
Imesimuliwa kutoka kwa Ma’qil ibn Yaassar ambaye amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa alihi wa sallam) amesema: ((Mmoja wenu kudungwa kichwa kwa sindano ya chuma ni bora kwake kuliko kumgusa mwanamke asiyeruhusiwa kwake)) [At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh Al-Jaami’]


Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
“Mwenye kuugusa mkono wa mwanamke bila ya kuwa na uhusiano wa kisheria naye (mahram yake), ataekewa kaa la moto kwenye kitanga chake cha mkono Siku ya Qiyaamah” (Fat-hul Qadiyr).

Mama wa waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) amesema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikubali Bay‘ah ya wanawake kwa mdomo tu bila kushikana mikono. Hakika hakugusa mkono wa mwanamke ambaye si mkewe (al-Bukhaariy).


Ni wazi kuwa katika Baiyah ya kwanza, waliyomuahidi kwayo Ma-Answaar waliokuwa wanaume watupu inajulikana katika Siyrah kama Bay‘ah ya kike kwani walitakiwa waahidi kama yale ya wanawake waliokuja baadaye, tofauti yake ni kuwa wanaume walimpatia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mikono yao. Allaah Anasema:
“Ewe Nabii! Wanapokujia wanawake walioamini wanakuahidi ya kwamba hawatamshirikisha Allaah na chochote, wala hawataiba, wala hawatazini, wala hawatawaua watoto wao, wala hawataleta uzushi wanaozusha tu wenyewe baina ya mikono na miguu yao, wala hawatakuasi katika jambo jema, basi peana ahadi nao na uwatakie maghfira kwa Allaah. hakika Allaah ni Mwingi wa maghfira, Mwingi wa rehema” (60: 12).
Akasema ‘Aaishah: yeyote katika waumini wanawake aliyekubali hayo na akapasi walipokubali Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaambia: ((Nendeni kwani mmetimiza kiapo cha utiifu)) Hapana! Naapa kwa Allaah, mkono wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haukugusa mkono wa mwanamke yeyote bali walitoa viapo vyao vya utiifu kwa maneno pekee”. Kisha ‘Aaishah akasema: “Naapa kwa Allaah, Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokea viapo vya utiifu kwa njia Aliyoitolea sheria Allaah na mkono wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) haujapata kugusa mkono wa mwanamke yeyote. Alipofungamana nao viapo vya utiifu alisema: ((Nimekubali kiapo chako cha utiifu [kwa matamshi])) [Muslim]

Vile vile:
عن أميمة ابنة رقيقة قالت : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : ((إني لا أصافح النساء)) رواه النسائي وابن ماجه وصححه الألباني " صحيح الجامع
Imetoka kwa Umaymah bint Raqiyqah ambaye amesema: “Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakika mimi sisalimiani na wanawake kwa kupeana nao mkono) [An-Nasaaiy, Ibn Maajah na imepewa daraja ya Swahiyh na Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyh al-Jaami’]
Tunatumai kuwa dalili hizo zitakuwa ni mafunzo miongoni mwa ndugu zetu ambao wana tabia hii ya kuamkiana kwa mikono na wanaume wasio mahram wao ili wabakie katika radhi za Mola wao na pia kuepukana na madhara yake.

((وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا))
((Na anachokupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho)) [Al-Hashr: 7]

Wa Allaahu A'alam
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْكSubhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM
IMETAYARISHWA NA ABUDUJANA arms1423@hotmail.com
Usinisahau kwenye dua zako
INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM

Tuesday, June 9, 2009

KUAMRISHANA MEMA NA KUKATAZANA MAOVU NI LAZIMA KWA KILA MUISLAMU

بسم الله الرحمن الرحيم

SUNNAH BAADAL ASRI
(HIZI NI HADITH KWA UFUPI TU )
مشروعية صلاة ركعتين بعد العصر (تذكير أهل السنة الحريصين على إحياء السنن و إماتة البدع

إن الحمد لله نحمده ونستعينه ونستغفره ، ونعوذ به من شرور أنفسنا وسيئات أعمالنا ، من يهده الله فلا مضل له ، ومن يضلل فلا هادي له ، وأشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله صلى الله عليه وسلم .
أما بعد
كان لا يدع ركعتين قبل الفجر , و ركعتين بعد العصر "
ALIKUWA MTUME صلى الله عليه وسلم HAWACHI KUSWALI RAKAA MBILI KABLA YA FAJRI NA RAKAA MBILI BAADAL ASRI
لألباني في " السلسلة الصحيحة " 6 / 101

حدثتني الصديقة بنت الصديق حبيبة حبيب الله المبرأة : أن رسول الله صلى الله عليه وسلم كان يصلي ركعتين بعد العصر
IMEPOKEWA KUWA MTUME صلى الله عليه وسلمALIKUWA AKISWALI RAKAA MBILI BAADAL ASRI
و هذا إسناد صحيح أيضا على شرط الشيخين ,
و قد أخرجاه من طريق أخرى عن مسروق مقرونا مع الأسود بلفظ : " ما من يوم يأتي علي النبي صلى الله عليه وسلم إلا صلى بعد العصر ركعتين ": "
HAKUNA SIKU ANAYOKUJA MTUME ILLA HUSWALI RAKAA MBILI BAADAL ASRI

ركعتان لم يكن رسول الله صلى الله عليه وسلم يدعهما سرا و لا علانية : ركعتان قبل صلاة الصبح , و ركعتان بعد العصر " .
و في رواية بلفظ
RAKAA MBILI ALIKUWA MTUME HAZIWACHI KUZISWALI KWA SIRI AU KWA DHAHIRI RAKAA MBILI KABLA YA SWALA YA ASUBHI NA RAKAA MBILI BAADA YA SWALA YA AL ASRI

و هو مخرج في " الإرواء " ( 2 / 188 - 189 ) و الذي قبله في " صحيح أبي داود " ( 1160
.و هنا ينبغي أن نذكر أهل السنة الحريصين على إحياء السنن و إماتة البدع أن يصلوا هاتين الركعتين كلما صلوا العصر في وقتها المشروع , لقوله صلى الله عليه وسلم : " من سن في الإسلام سنة حسنة .. "
MPAKA HAPA NAPENDA KUWAKUMBUSHA KILA ALIE NA PUPA YA KUHUISHA SUNNAH YA MTUME صلى الله عليه وسلم KILA ANAPO MALIZA KUSWALI AL ASRI KATIKA WAKTI WAKE AZISWALI RAKAA MBILI HIZI
من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo)) (Muslim

. و بالله التوفيق





اللهم اني أسألك علماً نافعاً و قلباً خاشعاً ولساناً ذاكراً

بسم ا لله ا لر حمن الر حيم
KUAMRISHANA MEMA NA KUKATAZANA MAOVU NI LAZIMA KWA KILA MUISLAMU.
Kwa hakika wale wanao penda uenee uchafu kwa walio amini, watapata adhabu chungu katika dunia na Akhera. Na Allah anajua na nyinyi hamjui
Na lau kuwa si fadhila ya Allah juu yenu na rehema yake, na kuwa hakika Allah ni mpole, mwenye kurehemu



SI HIYARI KUKATAZA MAOVU NI LAZIMA
Asema Allah
Haiwi kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapo kata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi . (Suratul Ahzab 36.)

Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu basi akiondoe (akibadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani)) Muslim.
Na kwa kuacha amri hii ya kuamrishana mema ndio matatizo na kila aina ya madhara yanatufika na kubwa zaidi mwenye kuacha kazi hii atakuwa na LAANAA NA DUA ZAKE HAIKUBALIWI

Asema Allah“Uharibifu umedhihiri barani na baharini kwa sababu ya yale iliyoyafanya mikono ya watu, ili Awaonjeshe (adhabu ya) baadhi ya mambo waliyoyafanya, huenda wakarudi (wakatubia kwa Mwenyezi Mungu)”.Ar Rum – 41Ikiwa athari ya uharibifu inafika barani na baharini, basi bila shaka itakuwa wepesi zaidi kwa athari hiyo kumfikia mwenye kutenda maasi hayo pamoja na watu walio karibu naye.
Na akasema Subhanahu wa Taala;"Na wanaoamini wanaume na wanaoamini wanawake, ni marafiki wao kwa wao. Huyaamrisha yaliyo mema na kuyakataza yaliyo mabaya”.At - Tawba – 71
UNAPO NYAMAZIA UOVU UTAPATA ADHABU ALLAH
Ndani ya Qurani tukufu pia tunakuta mifano mingi inayotujulisha juu ya umuhimu wa kuamrisha mema na kukataza maovu, na hapa nitautaja mfano mmoja wapo;Mayahudi katika dini yao walikatazwa siku ya Jumamosi wasijishughulishe na kazi yoyote ile isipokuwa wawe wanamuabudu Mwenyezi Mungu tu.Mwenyezi Mungu akataka kuwatia katika mtihani Mayahudi waliokuwa wakiishi katika kijiji kimoja cha wavuvi akajaalia iwe kila siku ya Jumamosi samaki wanakuja kwa wingi sana kuliko siku za kawaida.Wengine miongoni mwao wakashindwa kustahamili na wakaanza kuvua bila kuogopa, na wengine wakaona bora waipige chenga sheria hiyo ya Mwenyezi Mungu, wakawa siku ya Jumamosi wanakwenda kutega nyavu zao wapate kuwanasa samaki tu, lakini hawawachukuwi, mpaka siku ya Jumapili ndio wanakwenda kuwachukuwa.Baadhi ya watu wema miongoni mwao walikasirika tu, lakini hawakuwakataza wenzao wale waliokuwa wakivunja maamrisho ya Mwenyezi Mungu kwa kuipiga chenga siku hiyo ya Jumaamosi.Wengine wakawa wanawakataza wenzao, lakini wale watu wema walionyamaza wasikataze wakawa wanawaambia wenzao;“Kwa nini mnawaonya hali wao wanaelewa vizuri kuwa jambo hilo limekatazwa?”Basi ilipokuja adhabu ya Mwenyezi Mungu wakapata adhabu wale waliokuwa wakiasi na pia wale walionyamaza wasiwakataze wenzao. Ama wale waliokuwa wakiwakataza wenzao, wao walisalimika na adhabu hiyo.Mwenyezi Mungu anasema:“Na waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari: (watu wa mji huo) walipokuwa wakivunja (Sheria ya) Jumaamosi (ambayo waliambiwa wasifanya kazi katika siku hiyo wafanye ibada tu. Na kazi yao ilikuwa uvuvi). Samaki wao walipowajia juu juu siku za Jumaamosi zao: na siku isiyokuwa Jumaamosi hawakuwa wakiwajia (hivyo). Basi namna hivyo tuliwatia mtihani kwa sababu ya kuasi kwao.Na (wakumbuke wakati) baadhi ya watu katika wao waliosema (kuwaonya walovunja hishima ya Jumaamosi kwa kuvua na hali yakuwa wamekatazwa waliposema): “Pana faida gani kuwaonya watu ambao Mwenyezi Mungu atawaua au atawaadhibu kwa adhabu kali (papa hapa)?” Wakasema: “Tupate kuwa na udhuru mbele ya Mola wenu (kuwa tumeonya lakini hatukusikilizwa) na huenda wakaogopa.”Basi walipoyapuuza waliyokuwa wakikumbushwa tuliwaokoa wale walokuwa wakikataza maovu, na tukawatesa wale waliodhulumu kwa adhabu mbaya kabisa kwa kuasi kwao.Na walipotakabari wasiache waliyokatazwa tuliwaambia: “Kuweni manyani madhalilifu”.Al Aaraf – 163-166Katika aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema;“Na subirini, kwani Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa wanaofanya mema.Basi mbona hawakuwamo katika watu wa mbele kabla yenu watu wenye akili wenye kukataza uharibifu katika nchi? Isipokuwa wachache tu miongoni mwao ambao ndio tuliowaokoa.Na wale waliodhulumu (nafsi zao) walifuata waliyostareheshwa (maasi) na wakawa waovu”.Hud – 115-16Kwa ajili ya yote hayo Mwenyezi Mungu akatufaridhishia jukumu hili la kuamrisha mema na kukataza maovu na akawasifia Masahaba (RA) kuwa wao ni umma bora kupita umma zote kwa ajili ya kazi hii ngumu waliyoifanya kwa ukamilifu.


Mwenyezi Mungu anasema;“Nyinyi ndio umma bora kuliko uma zote zilizodhihirishiwa watu (ulimwenguni) – mnaamrisha yaliyo mema na mnakataza yaliyo maovu, na mnamwamini Mwenyezi Mungu..”Aali Imran – 110Na akasema;“Na wawepo katika nyinyi watu wanaolingania kheri (Uislamu) na wanaoamrisha mema na wakakataza maovu. Na hao ndio watakaotengenekewa”.Aali Imran – 104Na Mtume (SAW) akasema;"Maneno ya mwanadamu yote ni dhidi yake isipokuwa Kumtaja Mwenyezi Mungu au kuamrisha mema au kukataza maovu".Imepokelewa na Ibn Mardawea na kusimuliwa na Um Habiba (RA).WALLAHI MTAAMRISHA MEMAMwenyezi Mungu anasema;“Walilaaniwa wale walokufuru miongoni mwa wana wa Israili kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakipindukia mipaka (sana).Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya”.Al Maidah – 78-79Katika kuifasiri aya hii Mtume (SAW) alisema;“Mwanzo wa kuingia upotofu katika watu wa Bani Israil, ilikuwa mtu anapokutana na mwenzake (akimuona anafanya maasi) anamkataza kwa kumwambia;“Ewe mwenzangu muogope Mwenyezi Mungu na uache unayoyafanya kwani si halali kwako (kufanya hayo), kisha anaonana naye siku ya pili yake (mtu huyo) akiwa katika hali yake ile ile (akiwa anaendela na maasi yake), jambo hilo halimfanyi akaacha urafiki naye wala kuacha kula pamoja naye wala kuacha kukaa pamoja naye. Basi walipofanya vile, Mwenyezi Mungu akazipiganisha nyoyo zao baina yao”.Kisha Mtume (SAW) akaisoma aya hii;“Walilaaniwa wale walokufuru miongoni mwa wana wa Israili kwa ulimi wa Daudi na wa Isa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakipindukia mipaka (sana). Hawakuwa wenye kuzuiana (kukatazana) mambo mabaya waliyokuwa wakiyafanya. Uovu ulioje wa jambo hili walilokuwa wakilifanya”.Kisha akasema;“La si hivyo Wallahi! (mkitaka mistake na nyinyi) Mtaamrisha mema na mtakataza maovu, kisha mtamshika mkono yule aliyejidhulumu, na kumuongoza katika haki na mtamfunga ndani ya haki, ama sivyo Mwenyezi Mungu atazipiganisha nyoyo zenu pia, kisha atakulaanini kama alivyowalani”.Attirmidhy - Abu Daud na wengine.

Thursday, February 12, 2009

Maulid











Maulid
(Celebrating the Prophet Muhammad's Birthday)
According to Quran and Sunnah Only
منهاجنا: عَوْدَةٌ إلى الْْكِتَابِ والسُّنَّة بِفَهْمِ سَلَفِ الأُمَّة

$2500 REWARD

To the first 3 persons who can show Anywhere in Quran or Authentic Sunnah That the Companions of Prophet Mohammed (sallallahu 'alaihi wa sallam)
Annually Celebrated the Rasool's Birthday
.

Email:- arms1423@hotmail.com for your reward

And when it is said to them: 'Follow that which Allaah has sent down', they say: 'Nay, we shall follow that which we found our forefathers (following).' Would they do so even if the Devil invites them to the torment of the Fire?" [Surah Luqmaan: 21]






Prophet (sallAllaahu 'alayhi wa sallam) from numerous paths of narration that he said:I have not left anything that will bring you closer to Allaah and distance you from the Hellfire, except that I have commanded you with it. And I have not left anything that will bring you closer to the Hellfire and distance you from Allaah except that I have forbade you from it.” So there has not been left any room for amending anything from it, whether it be a simple or a trivial thing being amended.






Saalim ibn 'Abdullaah ibn 'Umar, who said: "I was sitting with Ibn 'Umar (radhi-yAllaahu 'anhu) in the mosque once, when a man from the people of Syria came to him and asked him about continuing the 'Umrah onto the Hajj (known as Hajj Tamattu'). Ibn 'Umar replied, 'It is a good and beautiful thing.' The man said: 'But your father (i.e. 'Umar ibn al-Khattaab) used to forbid it!' So he said: 'Woe to you! If my father used to forbid something which the Messenger of Allaah (sal-Allaahu 'alayhe wa sallam) practised and commanded, would you accept my father's view, or the order of the Messenger of Allaah (sal-Allaahu 'alayhe wa sallam) ?' He replied, 'The order of the Messenger of Allaah (sal-Allaahu 'alayhe wa sallam).' He said: 'So go away from me.' Ahmad (no. 5700) related similarly, as did at-Tirmidhee (2/82) and declared it saheeh..






This is why it is reported on the Imaam of Daar-ul-Hijrah (Madeenah), Imaam Maalik Ibn Anas, may Allaah have mercy on him, that he said: "Whosoever introduces into Islaam an innovation, which he deems is good (bid’atul hasanah), then he has claimed that Muhammad (sallAllaahu 'alayhi wa sallam) has betrayed (the trust of conveying) the Message. Read the saying of Allaah, the Mighty and Majestic: 'This day I have completed your Religion for you, and I have perfected My favor upon you, and I am pleased with Islaam as a Religion for you.' [Surat-ul-Maa’idah: 3]





So whatever was not (part of) the Religion on that day, is not (part of) the Religion on this day. And the last part of this ummah (nation) will not be rectified, except by that which rectified its





"So imitate (them Sahaba ) if you are not among them





Verily, imitating the righteous ones is success."

اللهم اني أسألك علماً نافعاً و قلباً خاشعاً ولساناً ذاكراً

رب اغفر لي ولوالدي، رب ارحمهما كما ربياني صغيرا

HATUFANANI NA WAHINDI





























Wednesday, February 11, 2009



{ قُلْ إِنْ كُنْتُمْ تُحِبُّونَ اللَّهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّهُ }
Sunnah Nzuri Katika Uislam
((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه

SWALI: ((Atakayefanya Sunnah njema atapata ujira wake na ujira wa yule atakayefanya kile kitendo mpaka siku ya Kiyama))
Je, kwanza hii ni Hadithi (Sahihi?) Pili, kama ni hadithi (Sahihi) je, Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa sallam) aliacha jambo (la Sunnah) kwetu ambalo hakulifanya yeye ili mtu alifanye katika Uislam?? Tunaomba utufahamishe kwa kutufafanulia wazi jambo hili.
Anajibu Aliekuwa Mufti wa Saudia Shaykh 'Abdul 'Aziyz bin Baaz Rahimahullah .
JIBU:

Hadithi hii ni Sahihi nayo inatuonyesha sheria (au kuruhusu) kuhuisha Sunnah na kuiitikia (kuifundisha) na kuhadharisha Bid'ah na shari. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema
((من سن في الإسلام سنة حسنة كان له أجرها وأجر من عمل بها من بعده لا ينقص ذلك من أجورهم شيئاً ومن سن في الإسلام سنة سيئة كان عليه وزرها ووزر من عمل بها من بعده لا ينقص من أوزارهم شيئاً)) خرجه مسلم في صحيحه
((Atakayefanya kitendo chema katika Uislam atapata ujira wake na ujira wa yule atakayekitenda baada yake bila ya kupungukiwa thawabu zao. Na atakayetenda kitendo kibaya katika Uislam atabeba (mzigo wa) dhambi zake na dhambi za yule atakayetenda wala hapungukiwi kitu katika (mzigo wa) dhambi hizo)) (Muslim)
Mfano wa hadithi hii iliyotoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema:
(( من دعا إلى هدى كان له من الأجر من أجور من تبعه لا ينقص من أجورهم شيئاً ومن دعا إلى ضلالة كان عليه من الإثم مثل آثام من تبعه لا ينقص ذلك من آثامهم شيئاً)) مسلم
((Atakayefanya daawa kuonyesha uongofu atapata thawabu (ujira) wa yule atakayemfuata bila ya kupungukiwa chochote katika thawabu zao na atakayeongoza katika upotofu atapata dhambi mfano wa dhambi zayule atakayefuata bila ya kupungukiwa chochote katika dhambi zao)) Muslim
Maana ya (Atakayefanya Sunnah katika Uislam) ni kuihuisha (kuifufua) Sunnah, kuidhihirisha na kuifichua Sunnah ambayo imefichika kwa watu (au imeghafiliwa na watu) basi huidhihirisha na kuibainisha, basi hupata thawabu kama za atakayetenda kitendo hicho na si maana kwamba ni kuzusha (kuanzisha) kitendo kipya. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kakataza kuzusha bid'ah akasema: “Kila uzushi ni upotofu” Na maneno ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na Ahlul-Ilm yanawafikiana yote pamoja wala hayapingani au kugongana.
Kwa hiyo, ilivyokusudiwa katika hadiyth ni kuihuiisha Sunnah na kuidhihirisha. Kama mfano wa kuwepo mwenye elimu katika nchi ambayo hakuna mafunzo ya Qur-aan au hakuna mafunzo ya Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) yeye akayarudisha mafunzo hayo kwa kuwakalisha watu na kuwafundisha Qur-aan na Sunnah au kuwaekea walimu kuwandisha watu elimu hizo. Au mfano mwingine akakuta katika nchi watu wanayoa ndevu zao au wanazikata akaamrisha wafuge na wasinyoe, hivyo atakuwa ameihuiisha Sunnah hii tukufu katika nchi hiyo ambayo watu walikuwa hawaijui au imeachwa na hadi kusahaulika au kutojulikana, na akapata thawabu sawa na thawabu za watakaopata hidaaya kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa sababu yake.
Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema
(( قصوا الشوارب وأعفوا اللحى وخالفوا المشركين)) متفق على
((Kateni masharubu na wacheni ndevu, muwe tofauti na washirikina))
(Hadiyth hii imesimuliwa na Al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhumaa)
Na watu walipomuona huyo mwalimu yeye mwenyewe kaziweka ndevu zake wakamfuata, kwa hiyo anakuwa kawahuiishia wao hiyo Sunnah. Nayo ni Sunnah ya waajib haifai kuiacha kwa kufuata maamrisho ya hadiyth iliyotajwa hapo juu na maana yake, akawa kwa kufanya hivyo, kapata thawabu sawa na thawabu zao.
Au mfano katika nchi watu hawaswali Swalah ya Ijumaa kutokana na kutokujua kwao (umuhimu wake) akawafundisha na kuwaswalisha akapata mfano wa thawabu zao pia. Na hivyo hivyo watu katika nchi nyingine hawatambui Swalah ya Witr akawafundisha wakamfuata au mifano kama hiyo katika vitendo vya ibada na sheria vinazojulikana katika Uislam, akazidhihirisha baada ya kufichika au kutokutambulika katika baadhi ya nchi au jamii ya watu.
Hivyo, atakayezifufua baina yao akazieneza na kuzibainisha ndiye yule aliyekusudiwa katika Hadithi kuwa 'kafanya Sunnah katika Uislam Sunnah njema’ kwa maana kwamba ameidhihirisha (fundisho, hukumu ya sheria ya Kiislamu. Ndio akawa miongoni mwa wale ((atakayefanya kitendo cha Sunnah njema katika Uislamu ))
Na sio maana kwamba aanzishe (azushe) jambo katika dini lisiloamrishwa na Allaah. Kwani uzushi ni upotofu kutokana na kauli ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hadithi sahihi,
(( وأياكم ومحدثات الأمور فإن كل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة))
((Jihadharini na mambo ya uzushi kwani kila uzushi ni Bid'ah na kila Bid'ah ni upotofu))
Vile vile anasema Mtume ((Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika hadithi Sahihi:
(( من عمل عملاً ليس عليه أمرنا فهو رد)) البخاري
((Atakayetenda kitendo kisichokuwa chetu basi kitarudishwa.)) Al Bukhari.
Na katika kauli nyingine,
( من أحدث في أمرنا هذا ما ليس منه فهو رد) متفق عليه.
((Atakayezusha katika mambo yasiyokuwa yetu basi kitarudishwa))
Al-Bukhaariy na Muslim.
Na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisema katika Khutba ya Ijumaa,
((أما بعد فإن خير الحديث كتاب الله وخير الهدى هدى محمد صلى الله عليـه وسلم وشر الأمور محدثاتها وكل بدعة ضلالة)) خرجه مسلم في صحيحه
((Amma Ba'ad hakika lililokuwa bora kabisa la kuhadithia ni Kitabu cha Allaah, na uongofu ulio bora ni uongofu wa Muhammad ((Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na jambo la shari kabisa ni uzushi wake na kila uzushi ni upotofu))
Muslim katika Sahihi yake.
Kwa hiyo aina ya ibada yoyote isiyoletwa na Allaah, haifai (kuifundisha) kuifanyia daawa, wala anayeileta na kuifanya hapati thawabu bali itakuwa kuitenda na kuileta kwa watu ni Bid'ah na huyo atakayeileta (kwa kuitangaza na kuieneza kwa watu) atakuwa ni katika yule anayeongoza katika upotofu na Allaah (Subhaana wa Ta'ala) Amemlaumu na kumhoji huyo mtu mwenye kutenda hivyo kuwa je,

Kwa kumalizia ewe ndugu yangu hadith yasema man-sannah si manibtada’a, fil islam sunnatal hassanah (yaani katika uislam na bid’a si katika uislam كل محدثة بدعة وكل بدعة ضلالة Kila bid’a ni upotofu na kila upotofu motoni) na lengo la hadith hii ni swadaqah na swadaqa ni sunnah zimepokewa hadith nyingi kuihusu swadaqah ndio Mtume akasema hadith hii na ndio maswahaba wakaelewa hivi:-
Ibn Umar (radhiallaahu ‘anhu) amesema: “Kila jambo la uzushi ni upotofu,
hata kama watu wataliona kuwa ni jambo zuri.” [Imepokewa na Abu
Shaamah na. 39]



((Au hao wana miungu ya kishirikina waliowatungia dini asiyoitolea idhini Mwenyezi Mungu…)) [Ash Shuura:21]
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك

Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka

Hukumu Ya Valentine Katika Uislamu

Hakika sifa zote ni za Mwenyezi Mungu ambae ameumba mbingu na ardhi
Ndugu zangu katika imani kabla ya kuwapa hukmu ya siku kama hii ya Valentine hatuna budi kujua ya kua sisi wa Islamu tuna mambo yetu na siku kuu zetu kulingana na mfumo wetu wa ki islamu, nawao makafiri wana mambo yao na siku kuu zao kulingana na mfumo wao wakikafiri, nimakosa makubwa sisi waislamu kuingia au kushiriki katika mifumo yao ambao inaenda kinyume na itikadi yetu ya kiislamu ndipo makureshi walipokuja kwa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). kumuomba ashiriki katika mfumo wao wa kiibada Allahu Subhaana-hu Wa Ta'ala aliteremsha jawabu kutoka mbinguni moja kwa moja kuja kwa bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). awajibu na awaambie لَكُمْ دِينُكُمْ وَلِيَ دِينِ Yakua nyinyi muna mfumo wenu na mimi nina mfumo wangu. Ikiwa mfumo wenu una waruhusu kufanya hivyo basi mimi wangu hauniruhusu kufanya hivyo kwa hivyo ndugu zangu waislamu nilazima tukae tukijua na kuelewa yakua maadamu twai-shi na makafiri hawatoridhika kuishi na wao tukiwa tumeshikilia mfumo wetu wa kiislamu mpaka watajaribu kutughuri sisi kuutupa mfumo wetu wasawa na kufuata mfumo wao muovu kama vile anavyo tuelezea Allahu Subhaana-hu Wa Ta'ala akisema kwenye qurani tukufu
وَلَن تَرْضَى عَنكَ الْيَهُودُ وَلاَ النَّصَارَى حَتَّى تَتَّبِعَ مِلَّتَهُمْ
Kwamba hawatoridhika mayahudi na manaswara mpaka tuwe ni wenye kufuata mfumo wao, ndipo bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). akatutaha-dharisha na kuwaiga wao au kujifananisha nawao ili tusiwe kama wao tukatupa uislamu wetu. Akasema Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam).
عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهماأن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
ليس منا من تشبه بغيرنا لاتشبهوا باليهود ولا بالنصارى }الترمذي{
Imepokewa na Abdillah ibn Omar (RadhiaAllahu Anhu)kwamba bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). amesema si miongoni mwetu sisi ambae ana jifananisha na wasio kua waislamu musijifa-nanishe na mayahudi wala manaswara. (tirmidhi)
Kwa hivyo katazo hili limekuja moja kwa moja kwa waislamu hatuna budi kukatazika na katazo hili la Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). isije ika-tufikia sisi adhabu kali itokao kwa Allahu Subhaanahu Wa Ta'alae kwa sababu ya kukhalifu amri ya bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). kama anavyosema Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala kwenye qurani tukufu
فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
“wajitahadhari wale wanao enda kunyume na amri ya bwana Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). isije wafikia wao balaa kubwa kutoka kwa Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala au adhabu iliyo kali”. Kwa hivyo haina haja sisi kujiingiza katika sikukuu zao kama hizi za laana zenye kuchangia maasi na munkarati tofauti kama unywaji wa tembo na uzinifu bali tutosheke na siku kuu zetu alizokuja nazo Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). Kuhusu siku kuu zetu twaelezewa kwenye hadithi kama hii
عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: كان لأهل المدينة في الجاهلية يومان في كل سنة يلعبون فيهما فلما قدم النبي صلى الله عليه وسلم المدينة قال: كان لكم يومان تلعبون فيهما وقد أبد لكم الله بهماخيرا منهما يوم الفطر ويوم الأضحى
Imepokelewa na Anas bin Malik (RadhiaAllahu Anhu) akisema kulikua kwa watu wa madina katika zama za ujahili sikumbili kila mwaka wakicheza ndani yake na kusherehekea. Alipofika Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). mji wa madina aliwaambia watu wa mji wa madina ya kua mulikua na siku mbili mukicheza ndani yake naku-sherehekea na Allahu Subhaanahu Wa Ta'ala amewabadilishia siku mbili hizo kwa siku mbili bora za Idi nazo ni siku kuu ya Idul’fitri na siku kuu ya Idul’adh’ha Kwa hivyo ndugu muislamu kwa hadithi hii twapata kuona yakua Uislamu pia una siku kuu zake ambazo zimewekewa waislamu waweze kusherehekea na kufura-hia zinapofika siku kuu kama hizo. Kwa hivyo haifai kwetu sisi kujiingiza kwenye siku kuu zao kama hizi ambazo zinaenda kinyume na mfumo wetu wa kiislamu. Kwa sababu lau sisi waislamu tutaziangalia siku kuu zao kama hizi kwa mtizamo wa kisawa sawa tutaona yakua ni siku kuu zenye kuleta uharibifu mku-bwa kwenye mujtamaa wetu wa kislamu. Si chrismas si valentine si pasaka day au happy new year hizi zote ni siku kuu ambazo zinaenda kinyume na Uislamu na kukhalifu muongozo sahihi wa Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). tuchukue mfano mdogo wa siku kuu kama hii ya valentine twaona yakua ni siku kuu ambao ina shajiisha uzinifu na kuupa nguvu kwa kila njia nakuweza kuhimiza kila mtu awe na wake. Siku kama hi asipite patupu. Yani maana yake mvulana awe na girlfriend na msichana vile vile awe na boyfriend ili wapate kufanya mapenzi yao ya kiholela holela wakiita siku kama hii ya kua ni siku ya wapendanao ili watimize haja zao za kimapenzi. Natija inao patikana siku kama hii ni kuleta uharibifu kwenye umma na magonjwa mabaya ya nao tokea-na na vitendo vibaya vya uzinifu na ndipo Mtume (Sallallaahu 'alayhi wasallam). akasema
kwenye kauli yake
ماظهرت الفا حشة في قوم حتى يعلنوا بها إلاابتلوا بها با لطوا عين والأوجاع لم تكن في أسلافهم الذين مضوا من قبل
Yakua “Hapa tadhihiri uovu kwenye watu mpaka wakawa wanautangaza isipokua mwenyezi mungu atawapatia mtihani wa ugonjwa wataun yani kwa lugha nyengine leprosy na njaa kali ambao mambo hayo haya kua kwenye umma ulio tangulia”. Na hii ndivyo twaona magonjwa mabaya yalivyo enea kwenye ulimwengu kama huu ambao umma uliyo pita hawa kupata magonjwa kama haya ya leo.
Ndugu muislamu sidhani kwamba kuna mtu asiejua kisa cha valentine ama sababu kubwa makafiri kuweza kusherehekea siku kama hii ambao inakuja kila mwaka tarehi 14 February.
Kwa ufupi katika karne ya tano kanisa la catholic church lilitaka kubadilisha mila au desturi ya kiromani ambao kuanzia karne ya nne, wa kiristo wote walikua wa kiifuata mila yenyewe ilikua kila unapo fika mwezi wa February vijana wote walio fikisha umri wa kubaleghi wanajitolea kwa kasisi wao LUPERIUS wakitia majina yao kwenye bahati nasibu na wasichana pia wakifanya hivyo hivyo kuingiza majina yao kwenye bahati nasibu. Kisha baadae jina la mvulana lililoebu-ka, mshindi hufuatilizwa na jina la msichana alietoka mshindi kwenye wasichana wenzake na kulazimwishwa kuishi pamoja mvulana huyu na msichana huyu wakiwa wanazini pamoja kwa mda wa mwaka mmoja, ama mpaka urudi tena mwezi huu wa february wafanyiwe tena bahati nasibu nyengine wa angaliwe kama ita wabakisha waendelee kuishi pamoja kwa njia ya uzinifu au ita watenganisha kila mtu atafute mwenzake mwegine waanze kuishi pamoja wakiwa wanazini pamoja kupitisha kipindi kama hicho.
Kisha wa catholic walichukizwa na mila kama hiyo wa kaamua kumuondosha kasisi kama huyo kwa jina LUPERIUS Nakumuwe-ka kasisi mwegine kwa jina VALENTINE. Kasisi wakimape-nzi ambae pia yeye aliuliwa kwa kosa la kukhalifu amri ya mfalme wake CLAUDIUS. Mfalme huyu alipata tabu kubwa sana kwa wanajeshi wake waliyokua wame-oa kwa sababu walikua wakikataa kwenda vitani na kuwaacha wakezao majumbani. Ikabidi mfalme kama huyu akataze watu wake kuoana na kuwaruhusu waishi hivi hivi kwa njia ya uzinifu peke yake ili patokeapo amri ya watu kwenda vitani pasitokezee tena matatizo kama haya. Kasisi huyu wa valentine, akawa yeye yuwa fungisha watu ndoa za siri nje ya kanisa kwa ajili ya kutimiza maslaha yake na kutimiza moja wapo katika maju-kukumu yake kama kasisi au kama kiongozi wa kanisani. Mfalme wake alipo pata khabari kama hizi kuhusu kasisi huyu Aliamrisha ashikwe atiwe jela. Alipotiwa jela alikua ameshaanza mapenzi na msichana mmoja wa mkuu wa magereza. Ikabidi kabla ya kifo chake amuandikie msicha-na huyu Barua ampelekee Barua yenyewe ilikua imeandikwa na Damu akimuambia Barua hii yatoka kwa Valentine wako Aki-kusudia mpenzi wako na hi ndio sababu wakiristo ama makafiri wakawa siku hi 14 february wanavaa nguo nyekundu au kupe-lekeana mauwa mekundu (Red Rose). Sikwa sababu kua hawana nguo nyengine zaku vaa isipokua hizo wala hakuna mauwa mengine Dukani kununua kupelekeana Isi-pokua red rose laa bali ni kuiga na kunasibisha barua hii iliyo andikwa na Damu. Sasa ndugu muislamu siku kama hii ina mafu-ngamano gani na itikadi yako ya kiislamu mpaka ukawa unashere-hekea siku hi na kujifananisha nawao kuva nguo nyekudu au hujui Mtume S.A.W amesema mwenye kujifananisha nawatu fulani na yeye huwa kama wao kwa hivyo ndugu muis’lamu tusi-kubali kughuriwa nawao kwa tashwishi zao wanazo tushawishi nazo kwa sababu wao makafiri wanatamani sisi tutupe mismamo yetu yadini ili nasisi tuwe kama wao gora mmoja kama anavyo tu-elezea mwenyezi mungu nakutu fahamisha kwenye Qurani Akisema
ودوا لو تكفرون كما كفروا فتكونون سواء
kwamba makafiri wanatamani mno nyinyi wa is’lamu mukufuru kama wao walivyo kufuru mupate kua sawa sawa nawao ili mu siwe na misimamo yoyote yadini ye nu,
na sisi leo tumekua twa enda na wao popote wanapo enda na popote pale wa ingiyapo tuko nawao pasina ya ku jifahamu na ndipo bwana Mtume S.A.W Akabashiri habari hizi na kuziele-za kwenye hadithi Akisema
عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم :لتتبعن سنن الذين من كان قبلكم شبرا بشبر وذراعا بذراع حتى لو دخلوا في جحر ضب لتبعتموه {متفق عليه}
“Anasema Abu said Al-khudhriy (R.A) kuwa Mtume S.A.W Alise-ma yakua mutakuja kufuata nyendo zawalokuja kabla yenu shubiri kwa shubiri na mkono kwa mkono mpaka watakapo ingia kwenye shimo la kenge bado muta wafuata” Kwa haya machache tumuombe Allah atupe fahamu ya Dini yetu na athibitishe nyoyo zetu kwenye misimamo ndani ya Dini yetu na atuonyeshe haki kua ni jambo zuri na atuwezeshe kuifuata Na atuonyeshe batili kua nijambo baya Na atuwezeshe kuiyepuka.
Wa Billahi Tawfiq.
سُبْحـانَكَ اللّهُـمَّ وَبِحَمدِك، أَشْهَـدُ أَنْ لا إِلهَ إِلاّ أَنْتَ أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتوبُ إِلَـيْك

Subhaanaka Allaahuumma Wa Bihamdika, Ash-Hadu An Laa Ilaaha Illa Anta, Astaghfiruka Wa Atuubu Ilayka
TUSISAHAU KUWA TUTAULIZWA TULIFANYA NINI KATIKA KUULINGANIA UISLAM
ABUDUJANA arms1423@hotmail.com
رب اغفر لي ولوالدي، رب ارحمهما كما ربياني صغيرا


Usinisahau kwenye dua zako
INSHAALLAH TUWE MABALOZI WA UISLAM

اللهم اني أسألك علماً نافعاً و قلباً خاشعاً ولساناً ذاكراً
لا تنسوا إخوانكم في فلسطين والعراق وفي كل مكان بالدعاء

اللَّهُمَّ قَدْ تَدَاعَى اليَّهُودُ وَأَعْوَانُهُمْ عَلَى إِخْوانِنا الْمُسْلِمِينَ فِي فِلِسْطِينَ حَتَّى أَهْلَكُوا الْحَرْثَ وَالنَّسْلَ، وَلاَ نَاصِرَ لَهُمْ مِنْ دُونِكَ، وَلاَ كَاشِفَ لُغُمَّتِهِمْ سِوَاكَ فَاجْعَلْ لَهُمْ مِنْ هَذَا الكَرْبِ فَرَجاً وَمَخْرَجاً وَأَيِّدْهُمْ بِنَصْرٍ مِنْ عِنْدِكَ وَادْحَرْ عَدُوَّهُمْ وَتَقَبَّلْ شُهَدَاءَهُمْ وَأَخْلِصْ نِيَّاتِهِمْ يَا رَبَّ العَالَمِينَ.